PATA MAKALA NZURI KWA AFYA YAKO KWA KUANDIKA TAARIFA ZAKO MUHIMU KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI

PATA MAKALA KWA AJILI YA AFYA YAKO KWA KUWEKA TAARIFA ZAKO HAPA

* indicates required

Ijumaa, 16 Juni 2017

MANUFAA YA MAJANI YA MPERA KWA AFYA YAKO





 Image result for majani ya mpera
MAJANI YA MPERA

FAIDA 17 ZA KUTUMIA MAJANI YA MPERA(GUAVA LEAVES).
Habari yako rafiki yangu mpendwa ambae unaendelea kufuatilia Makala za afya. Siku ya leo ningependa kueleza kuhusu faida za kutumia mmea ambao umeonekana ni mmea wa kawaida ila unafaida nyingi katika afya yetu
Mapera ni matunda ya msimu yenye wingi wa vitamini A na C, madini ya potasiam, nyuzi nyuzi nzuri yani fiber na 'lycopene' vyote hivi ni muhimu kwa afya.
Watu wengi hutumia tunda tu pasipokujua si tunda pekee lenye manufaa kwa afya zao. Majani ya mpera ni mazuri sana kwa ajili ya kisukari,ngozi, nywele na afya yako kwa ujumla.

FAIDA ZA KUTUMIA MAJANI YA MPERA KWA AJILI YA AFYA YAKO.
1.Chai ya majani ya mpera inasaidia mwili kuwa stadi, inasaidia madini ya carbohydrates yasigeuzwe kuwa sukari ndani ya mwili hivyo kupunguza hamu ya kula.
2.Chai ya majani ya mpera pia inashusha kiwango cha sukari mwilini na kuzuia mwili kuondoa 'insulin'. Kwa sababu hii wagonjwa wa sukari wanashauriwa kuitumia mara kwa mara.
3.Chai ya majani ya mpera pia hupunguza lehemu mbaya(bad cholestrol) bila kudhuru lehemu nzuri.
4.Chai hii ina nguvu za kudhibiti vijidudu vya magonjwa mwilini hasa kuzuia magonjwa ya kuharisha na kipindupindu.
5.Chai hii inalinda mchafuko wa tumbo na pia inasaidia kukabili madhara yaletwayo na chakula chenye sumu.
6.Chai hii hutibu kukohoa na kupumua kwa tabu.
7.Upatapo uvimbe wa fizi na maumivu mdomoni kama jino kuuma, tafuna majani ya mpera.
8.Kwa matatizo ya homa ya dengue, chemsha glasi mbili na nusu na majani ya mpera (kadiria majani 9) mpaka maji yabakie nusu ya ujazo wa awali.
9.Chai ya majani ya mpera imefahamika kutibu kansa na 'prostate' kwa wanaume.
10.Chai hii inasaidia kwa wanaume wenye tatizo la kuzalisha (Infertility).
11.Ponda majani ya mpera na kuweka sehemu ya kidonda au iliyokatika kuondoa maambukizi. Kwa maumivu nje ya sikio tumia chai ya majani ya mpera. Tia matone ya chai hii iliyopoa kwenye sehemu iliyoathirika.
13.Majani ya mpera hupondwa na kupakwa eneo lenye muwasho uletwao na allergy.
14.Unapoumwa na wadudu majani yaliyopondwa ni tiba sahihi.
15.Majani ya mpera yana saidia kupigana na mba na chunusi kutokana na wingi wake wa vitamini C.
16.Kuondoa madoa meusi kwenye ngozi ponda majani ya mpera changanya na maji kiasi na upake badala ya dawa za kawaida.
17.Fanya kama namba16. kwa tatizo la ngozi kuzeeka mapema.
18.Majani ya mpera yanaondoa tatizo la kukatika kwa nywele. Chemsha majani kisha wacha yapoe na ukande kwenye paji na eneo la ngozi taratibu kwa dakika 15. Wacha kwa dakika 30 kisha osha na maji safi bila shampoo au sabuni. Fanya hivyo mara 3 kila wiki.
Wengi wananiuliza namna ya kuitengeza chai ya majani ya mpera. Kuna namna mbili. Aidha chemsha maji kama glasi nne mpaka itokote sana, chukua majani kama 10 ya mpera, weka ndani ya yale maji moto kisha funika kwa dakika 10 - 15 koroga, chuja, chai yako tayari. Aina ya pili ni chemsha maji hayo pamoja na majani yakiwa ndani. Ikitokota ondoa kwenye moto, wacha kwa dakika 10 -15 chuja, chai tayari. Waweza ukatumia majani yaliyo kauka pia.
Zingatia ukichanganya na asali badala ya sukari ndio bora zaidi.

Najua umepata kujifunza kitu rafiki yangu kama umependezwa na tiba hii ya leo share na marafiki zako na magroup mbalimbali
Pia kwa ushauri juu ya afya yako mpendwa wasiliana nami kwa
NAMBA 0652250418
WhatApp 0652250418⁠⁠⁠⁠

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni