PATA MAKALA NZURI KWA AFYA YAKO KWA KUANDIKA TAARIFA ZAKO MUHIMU KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI

PATA MAKALA KWA AJILI YA AFYA YAKO KWA KUWEKA TAARIFA ZAKO HAPA

* indicates required

Ijumaa, 16 Juni 2017

TAMBUA FAIDA ZA KAROTI KIAFYA



Image result for karoti 

KAROTI
 
Karoti na Tiba
Mwili wa binadamu ili kuwa na afya bora unahitaji virutubisho mbalimbali na ndio maana tunashauriwa kula mlo uliokamili ukijumuishwa na matunda na maji ya kutosha.

Virutubisho hivi hupatikana katika matunda, mboga za majani, samaki, nyama na vyakula vingine vingi. Watu wengi tunapenda kujumuisha karoti katika mapishi yetu au kama sehemu ya matunda lakini hatujui kwa undani faida zake. Hebu basi leo tuangalie faida hizo kwa pamoja;

Faida ya karoti
1.    Karoti husaidia kuboresha afya ya macho
Karoti inavirutubisho muhimu kwa afya ya macho, sio tu kuboresha uwezo wa kuona lakini pia kuyalinda macho kutonana na matatizo yanayotokana na uzee. Uwepo wa vitamin A katika karoti husaidia yote haya na kuyafanya macho yako kuwa yenye afya.

2.    Huboresha afya ya ngozi
Ulaji wa karoti husaidia kuboresha afya ya ngozi ya mtumiaji. Vitamin A iliyopo katika karoti haina faida katika macho tu bali pia husaidia kuifanya ngozi iwe ya kuvutia na kupendeza. Vitamin A huilinda ngozi na chunusi, halala na mabaka meusi yaliyopo kwenye ngozi. Kwa mujibu wa tafiti ya chuo kikuu cha Nottingham, ulaji wa matunda na mboga za majani husaidia afya ya ngozi kwa njia za asili kabisa.

3.    Husaidia mmeng’enyo wa chakula
Karoti ni chanzo kizuri cha nyuzi zenye virutubisho ambavyo husaidia kwa kiasi kikubwa katika umeng’enyaji wa chakula na kurahisisha mtumiaji kupata haja kubwa kwa urahisi. Karoti pia husaidia kupunguza tatizo la kutopata choo, husaidia kulikinga tumbo na magonjwa mbalimbali na husadia kuzuia kansa ya utumbo.

4.    Husaidia kuimarisha afya ya kinywa
Virutubisho vingi vinavyopatikana katika karoti husaidia kuimarisha afya ya mdomo. Ulaji wa karoti utaacha kinywa cha mtumiaji kuwa chenye harufu nzuri, fizi zilizoimara lakini pia zitamlinda mtumiaji na magonjwa mengi yanayopatikana katika kinywa.

5.    Husaidia kusafisha mwili
Karoti husaidia kusaga sumu zilizopo mwilini ktoka katika ini na kuzisafirisha katika kibofu na utumbo mkubwa ili ziweze kutolewa nje kwa njia ya mkojo na kinyesi. Uwepo wa vitamin A katika karoti husaidia kusukuma sumu hizo na kupunguza mafuta yasiyohitajika wakati huohuo nyuzi zilizopo katika karoti husaidia kusafisha utumbo na msukumo wa uchafu.

6.    Husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu.
Uwepo wa ‘carotenoids’ katika karoti husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Pia husaidia kusimamia glucose na sukari inayogeuzwa katika damu na kutumiwa na mwili ambapo husaidia mgonjwa mwenye kisukari kuishi maisha ya kawaida.

Karoti huweza kutumiwa kama kiungo katika chakula chako, huweza kuliwa kama tunda lakini pia unaweza kutengeneza juisi kutokana na tunda hili.

Kama ulikuwa hufahamu faida za karoti na umuhimu wake katika mwili wako basi anza leo kujumuisha karoti katika mwili wako, mwili haujengwi kwa matofari… bali kwa mlo ulio kamilika.⁠⁠⁠⁠ 
Kwa ufupi sana tunasema hivi;

🥕FAIDA 10 ZA MMEA WA KAROTI

🥕Karoti ina faida zifuatazo
🔸Ina ongeza uwezo wa macho kuona
🔸Inasaidia mwili kupambana na mgonjwa ya moyo
🔸Inasaidia mwili kupambana na Kansa 🔸Inaboresha afya kinywa cha mwanadamu
🔸Ina ongeza ilinzi wa INI ili lisiathirike na mgonjwa.
🔸Ina linda afya ya ngozi ya mwili wa binadamu
🔸Inasaidia kuboresha mfumo wa mmengenyo wa chakula
🔸Inasaidia kuzuia kiharusi
🔸Inadhibiti sukari katika damu
🔸Inasaidia mwili kutokuonyesha dalili za uzee mapema..yaani mwili kuchoka haraka 🔻Tutumie karoti kwa wingi kulinda afya zetu David Nghambi 0752090436/0652250418 kwa ushauri zaid 🥕🥕🥕⁠⁠⁠⁠

Maoni 7 :

  1. Saf sana kaka
    Together we can

    JibuFuta
  2. Habari, karoti ukiitafuna inaweza kupelekea mtu kupata typhoid?

    JibuFuta
  3. I real like the way it expressed about natural vegetables
    respect to all who made it

    JibuFuta
  4. Asante sana.nimeelewa,nikaelimika hakika karuti ni nzuri kwa afya bora kwa kila MTU.nashukuru.afya njema ni chakula.

    JibuFuta
  5. Everydays i will use karoti

    JibuFuta
  6. Elim nzur tujijenge kiafya kwa kutumia matunda

    JibuFuta