PATA MAKALA NZURI KWA AFYA YAKO KWA KUANDIKA TAARIFA ZAKO MUHIMU KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI

PATA MAKALA KWA AJILI YA AFYA YAKO KWA KUWEKA TAARIFA ZAKO HAPA

* indicates required

Ijumaa, 16 Juni 2017

LIJUE VIZURI TATIZO LA PRESHA (SHINIKIZO LA DAMU) NA NAMNA YA KULIKABILI



PRESHA (SHINIKIZO LA DAMU 

NJIA KUMI ZA KUDHIBITI PRESHA (SHINIKIZO LA DAMU) KWA KUTUMIA VITU ASILIA KABISA.Shinikizo la damu (presha) ni tatizo la siku nyingi ambalo lilikuwa likiwapata watu wenye umri mkubwa, lakini leo hii takriban asilimia 30% ya vijana duniani wanakabiliwa na tatizo hili.
Zaidi ya watu billioni moja duniani wanakumbwa na tatizo hili, ugonjwa huu ni hatari sana kwani husababisha madhara makubwa kwa mwanadamu ikiwemo;
1.Mshituko wa moyo (heart attack )
2. Kiharusi (stroke)
3. Kupanuka kwa moyo na hatimaye kufeli na mengineyo.
Madhara haya ni makubwa na yamesababisha watu wengi kuaga dunia. Kwa kutambua madhara yatokanayo na ugonjwa huu nimeamua kutumia mda wangu kuandika makala hii nzuri kwa ajili yako ndugu msomaji wa makala  za blogu hii ya daviddontz.blogspot.com

Njia hizi kumi (10) zitakusaidia kudhibiti presha yako na kufanya uishi mda mrefu hapa  duniani.

Zifuatazo ni njia kumi za kudhibiti presha au shinikizo la damu kwa kutumia vitu asilia visivyo na madhara kabisa kwa mtumiaji.

1. Tambua kiwango cha presha yako.
Hiki ni kitu cha kwanza unachotakiwa ukifanye kwani watu wengi hatuna utaratibu wa kucheki presha zetu, kwahiyo inabidi upime na kujua kiwango cha presha yakoo.

Presha hupimwa kwa namba mbili mfano 120/80 ambapo namba ya juu Systolic Blood Pressure(SBP) huonesha kiwango cha presha kinachotoka kwenye moyo kuingia kwenye mishipa ya damu
Namba ya chini Diastolic Blood Pressure (DBP) huonesha kiwango cha presha ambacho hutumika kupeleka damu katika ventriko ya kushoto

UCHAMBUZI WA PRESHA
1. Kawaida              < 120  
2. Hatari ya kupata  (120-139)
3. Presha daraja 1 (140-159)
4. Presha daraja 2. (>160)
Kwahiyo tambua uko group gani Kati ya hayo manne

2. Tumia vyakula vitokanavyo na mimea
Vyakula hivi huwa na mafuta kidogo na hivyo hukupa afya nzuri ya moyo na mishipa ya damu, tafiti zinaonesha utumiaji wa vyakula vitokanavyo na mimea hupunguza presha kwa kiwango cha 7/5 mmhg
vyakula hivi nimevigawa katika makundi manne kama ifuatavyo;
1. Nafaka
2. Mboga mboga
3. Jamii ya kunde
4. Matunda
Ukitumia vizuri makundi haya ya vyakula basi utaweza kudhibiti presha yako.

3. Punguza kiasi cha chumvi
Mtu mzima anahitaji <1500mg za chumvi kwahiyo jaribu kupunguza kiwango cha chumvi kwani figo hutumia chumvi (sodium) kama njia ya kupandisha presha.

4. Kula vyakula vyenye potassium kwa wingi
Unapotumia vyakula hivi mwili hupata kiwango kikubwa cha potassium, mtu mzima anahitaji 4700mg za potassium kila siku ili kuweza kupunguza presha mwilini, kwani figo hutumia potassium kushusha presha mwilini.
VYAKULA VIPI VINA POTASSIUM??
vyakula kama ndizi, nyanya na bidhaa zotee zitokanazo na nyanya, machungwa, mboga za majani, maharage nk.

5. Mazoezi
Tenga mda wa dakika 30 kwa siku kwa ajili ya mazoezi, mazoezi husaidia kupunguza uzito na kusafisha mfumo wa damu hivyo basi husaidia katika kushusha presha yako.

6. Punguza uzito
Uzito mkubwa ni chanzo cha magonjwa mengi yakiwemo magonjwa ya moyo kama vile presha hivyo basi punguza uzito wako kuepukana na tatizo hili.

7. Punguza utumiaji wa pombe au acha kabisa.
Pombe ikitumiwa kwa kiwango kidogo ni nzuri kwa afya mfano mwanamke anashauriwa atumie chupa moja tu kwa siku ( hatari ya kupata kansa ya matiti) na mwanamme atumie angalau chupa mbili kwa siku
Pombe kupita kiasi husababisha mafuta mabaya (LDL) kwenda kudeposit(kujikusanya)  kwenye mishipa ya damu na kufanya kupungua kwa ukubwa wa mishipa ya damu na kupelekea mtu kupata presha. Lakini hata hivyo mimi kama David Nghambi huwa sishauri mtu kutumia pombe.

8. Epuka uvutaji sigara au tumbaku
Kwani uvutaji sigara humuweka mtu katika nafasi ya kupata magonjwa ya moyo mara mbili zaidi ya yule asiyevuta.

9. Punguza msongo wa mawazo
Unapokuwa na msongo wa mawazo mwili hutoa adrenaline na cortisol homoni ambazo hufanya mishipa ya damu kusinyaa na kufanya damu kusafiri kwa kasi kubwa na hatimaye hupelekea mtu kupata presha.

10. dawa asilia zisizo na kemikali.
Kwa wale wote ambao hushindwa kupunguza presha zao kwa kutumia njia hizo 9 hapo juu au niwagonjwa wa siku nyingi huwa nawashauri watumie dozi ya presha ambapo atapatiwa  DAWA YA GINKARDIO  na kiondoa sumu maarufu chenye uwezo wa kurekebisha hormone na mifumo yote ya mwili. GINKARDIO  ni dawa asilia kabisa iliyotengenezwa kutokana na mti wa ginkgo na kuwekwa kitaalamu katika mfumo wa vidonge:
DAWA HII INA KAZI ZIFUATAZO
1. kuondoa mafuta na mabaki kwenye mishipa ya damu
2. huondoa oksijeni iloshindwa kutumika kwa mabaki haya ya hewa hii ni chanzo kikubwa cha presha na kansa mbalimbali
3. Humkinga mtu asipate madhara yatokanayo na presha
4. Huzuia damu isigande
5. Huzuia utengenezaji wa mabonge kutoka kwenye damu iliyoganda ambayo ndo chanzo kikubwa cha kiharusi (stroke )
6. husaidia kubalance damu inayokwenda kwenye moyo na ubongo.
NDUGU  YANGU KAMA UNA MATATIZO YA PRESHA  HUU NI UFUMBUZI KWAKO HUNA HAJA YA KUTESEKA NA KUHANGAIKA TENA  WASILIANA NAMI   KWA TIBA NA USHAURI JUU YA TATIZO HILI
DOZI NI SIKU 90 
NAMBA 0652250418/0752090436
WHATSAPP 0652250418
PIA LIKE PAGE YANGU SASA David Mshauri wa Afya  kwa elimu bora ya afya yako⁠⁠⁠⁠

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni